Monday, October 20, 2008

"Joseph Haule kwenda kwa Joseph Kabila"


Mwamba wa miondoko ya Hip Hop ndani ya Bongo Joseph Haule(Prof Jay) anatarajiwa kuondoka na kwenda inchi ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo yote ikiwa ni kwa ajili ya kwenda kupiga kampeni za kuomba kura za masela wa inchi hiyo katika tuzo za MTV Afrika(MTV AFRCA MUSIC AWARDS)

Tuzo hiyo ambayo pia itawashirikisha nyota wa mziki wa Hip Hop kutoka Marekani The Game pamoja na Lily Wayne inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Habari ambazo zilizothibitishwa na mwakilishi wa MTV ndani ya Bongo,Christine Mosha,zilisema kwamba washiriki wote watakwenda katika nchi walizopangiwa kwenda kuomba kura,ambapo mwakilishi wetu Prof Jay yeye alipangiwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo.

Watanzania wote tupo pamoja na Prof Jay..Tunamuomea mafanikio katika kinyang'anyiro cha tuzo hiyo.

2 comments:

Anonymous said...

mi ni mmoja kati ya watu wachache ambao hawamkubali sana Prof Jizze wa sasa...prof yule wa chemsha bongo na mamsap ndo wa haswahaswa ila huyu 'story teller' ananiboa mbaya!!..mi namuita 'babu' cuz amekuwa mpiga hadithi siku hizi!!..ni hayo tu....

Anonymous said...

mshkaji isije ukawa una beef na Prof Jay...Kua mkweli bwana na uweke pembeni maswala ya beef...Huyu jamaa ni bomba mbaya.