Ule usemi wa ukimuona kobe ameinama ujue anatunga sheria umejidhihirisha kwa msanii wa miondoko ya Bongo flava Robert Mangwea baada ya kutoka tena na kubamba kisawasawa.
"Sio kwamba sipendi misosi ya kumwaga,ma-pizza ma-barger na mazaga mazaga,ni kwa vile tu hatuna mahela"ni miongoni mwa mistari iliyomo katika mwimbo wake wa Nipeni dili uliomo katika album yake mpya ya Nge 1982 iliyomo na nyimbo nyingine kama Mida Mibovu,Singida Dodoma na She Performs aliyompa shavu TID ambazo tayari zimeanza kurushwa hewani.
Wimbo huu wa Nipeni dili umeonyesha kua Ngwea ni kichwa cha kuotea mbali kutokana na mashairi yake na uwezo mzima wa kutambaa na beat..Nipeni dili imeweza kujishika chati za juu katika vituo vingi vya redio hivi sasa.
Ngwea ambae ni mmoja wa wasanii kutoka katika kundi la Chamber Squad anatarajia kuingiza sokoni album yake ya pili baada ya kumalizika kupikwa.
Kama tutakumbuka albam yake ya kwanza ya Bado Nimo a.k.a mimi ili weza kutesa na vibao kama vile:Getho langu,Mikasi,Napokea Simu na vingine vingi.
Haya tunakungoja kaka kwa mwendo wa Nipeni dili Masela Tukakamate Mahela.
1 comment:
Ngwea mkali...hilo liko wazi...ila.....nitaongea baadae hii ila....
Post a Comment