Saturday, November 29, 2008

Huu Kweli Mwaka wa Shetani


E bwana ni moja ya makundi yanayotesa kwenye muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, mi mwenyewe ni mmojawapo wa ninaowakubali Nako 2 Nako lakini katika hali ambayo haikutegemewa na wapenzi wa muziki hapa Bongo kundi hili mahiri linaloundwa na wasanii Ibra da Hustler, Lord Eyez, G-Nako, Bu-Nako na Izzi-Nako limesambaratika juu chini.

Utafiti uliofanywa na Itajulikana hivi karibuni umebaini kuwa wasanii wa kundi hilo wamegawanyika vipande viwili na kila kimoja kuelekea upande wake kikubwa ikiwa ni kutoaminiana.

Ibra ametangaza kujitoa kundini sambamba na Bu-nako hali inayofanya Lord kubaki na G-Nako kwani Izzi hafahamiki yuko upande gani na huwa haonekani mara kwa mara.

Wasanii hao, wamekuwa wakimtuhumu kiongozi wao Lord Eyez kuwa ndie chanzo kikubwa cha mgawanyiko huo kutokana ubabe wake kimaamuzi.

No comments: