Saturday, December 6, 2008

Muumin Mwijuma Kurudisha Heshima Kwa Sweet Baby.



Mwanamuziki wa Dansi nchini Mwinjuma Muumin anatarajia kurudisha heshima kama ilivyo kipindi cha enzi ya"Tunda".
Mwanamuziki huyo ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya African Revolution aliambia Itajulikana kua yupo katika kambi na bendi yake kwa maandalizi makali ya ujio wa mfumo mpya ambao ameahidi utafunika mbaya muziki wa dansi na kuweza kurudisha heshima kama ilikua enzi ya nyimbo ya "Tunda"Kibao "Sweet Baby"amekitaja kua ni miongoni mwa vibao anavyoamini kua vitamrudisha tena na kua juu.
Haya kaka wapenzi wa muziki wanasubiri kwa hamu ujio huo.

No comments: