
Gwiji la muziki wa zouk nchini Stara Thomas anakuja kivingine baada ya kuamua kumpa shavu mkali na nyota wa miondoko ya 'Hip hop' Chid Benzi kutoka kundi la Lafamilia kwenye pini lake jipya liitwalo 'Nini sina". Kwa mujibu wa Stara ambaye ni mama wa watoto wawili kwasasa, anauhakika kazi aliyoifanya itabamba kwani nia na madhumuni yake ni kuwapa raha wapenzi wake waliokuwa na kiu ya kumsikia baada ya kimya kirefu.Akiendelea mdada huyu alisema tayari ameshaanza maandalizi kwa ajili ya video track hilo lenye maudhui ya kimapenzi..Haya Wadau Sikilizia Pina la Ukweli Hilo.....Si Kitoto....
4 comments:
Wabongo tutakua watu wa kubana kama hatujataja jina la Chid Benz kua ni miongini mwa viumbe waliofunika katika mindoko ya Hip Hop nadhani kwa East Africa nzima...Sina hakika lakini nadhani huyu jamaa anaongoza kwa kupewa shavu na wanamziki wengi this year!!Wafuatiliaji naomba mnisaidie katika hilo!!!Jamaa ni funiko bayaaaaa!!
sina hakika kama namkubali sana Chidi km watu wengine mnavyomkubali....kashirikishwa sana ths year,hilo liko wazi kabisa ila mi nadhani sio mkali kihiiiiivyoooooo....wa kawaida tu ila kismati anacho...wasiwasi wangu ni kwamba wabongo tukishachoka sauti yake(nadhani ndo inamuweka juu) si ndo basi tena tumempoteza?.kwa hilo ni wakati sasa aanze kubuni mavitu mengine ya kututeka!!
halafu jamaa kashirikishwa mpaka kwenye bolingo!!..sikutegemea....tunasubiri kuona aliyoyafanya na Stara...
Chid benz jamani sio wa kivile sana, ukitaka kugundua jamaa hana lolote angalia ni nyimbo ngapi katoa yeye kama yeye na zimekubalika?ila angalia akishirikishwa huyu atakuja kuisha vibaya sana,nadhani kama alivyosema hapo juu mshikaji jamaa ni sauti tu ila hana kipya zaidi...mimi naomba aige mifano ya kina AY au Prof Jay hawa jamaa ndio naamini ni mkali Bongo nzima....
mkali suala la wakali km kina AY sio wakuigwa....vile vipaji binamu!!..huyu dogo Chidi km nilivyosema, kismati tu...sasa ndo ajitajihidi azichange kabla jua halijachwa!!...
halafu jamani hivi kwa nini mastaa wa Bongo hawajali appearance zao?.kwa mfano, Q-Chief wakati anaanza alikuwa so sexy mpk nikampenda ila sasa,mh!!!.hv vitambi ndo washaona fashion?.
Post a Comment