

Ni wakati mwengine kwa Wabongo wapendao Burudani kupata Uhondo toka kwa wana Hip Hop waishio Unyamwezini(USA)nao si wengine ila ni mwanadada Eve na mzee mzima Fat Joe.Katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu Bongo imejitoa kua safu za nyuma katika swala la Burudani katika Africa kwa kuweza kuwaleta wanamuziki mbali mbali toka anga za kwa Obama.Kama tutakumbuka wanamuziki kama vile Akon,50 Cent wameweza kukanyaga ardhi ya bOngo na kufanya maonyesho ambayo yamekua yakimeza nyomi la kueleweka.Ni wakati mwengine redio ipendwayo ya Clouds Fm inawaletea wasanii wawili maarufu Eve na Fat Joe siku ya tarehe 8 December.
Kazi kwenu wapendao burudani waishio Bongo.
No comments:
Post a Comment