Wednesday, November 19, 2008

"Nature Aachiwa Kwa Dhamana".


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya(Bongo Flava)Juma Kassim maarufu (Juma Nature)amechiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na mizee(Polisi)baada ya kupatikana na shutuma za kujihusisha kimapenzi na binti wa chini ya umri wa miaka 18.

Sakata hilo lilimpata Nature baada ya binti huyo kupotea kwa siku nzima nyumbani kwao na ndipo wazazi walifuatilia waligundua kua binti huyo alikua akila raha na msanii Juma Nature.

Wazazi hao walichukua hatua ya kushtaki kwa mizee(Polisi)na bila ajizi walimtia mikononi.

Sasa mabinamu wa kweli hembu tukae chini tujiulize...Nini wanafanya wasanii wetu...Kazi ya sanaa pamoja na kuburudisha pia inaelimisha,,,Sasa ni elimu gani tuipatayo kwa mambo kama haya???Kama Nature kweli alifanya jambo hili basi liwe ni fundisho wa kwa wasanii wengine.Ni jambo la aibu.

No comments: