Tuesday, November 18, 2008

"Ngwea Kaanza Kukamata Mahela"


"Nipeni dili masela nikamate mahela".Ni miezi michache tu tangu mwanamuziki wa kizazi kipya toka kundi la Chamber Squard Albert Mangwea(Cow Boy)kuachia kitu cha Nipeni dili ambacho kinafunika vilivyo East Africa tayari Ameshanza kula mialiko ya show kibao za maana.
Ngwea aliongea na kusema kwamba kupitia mpini huo amerudi upya katika game huku akiwa anakamata mahela kwa kutokana na dili pamoja na show kibao.
"Nataka niwaonyeshe mashabiki wangu kwamba kimya kingi kina mshindo.Nilikua nikijapanga,sasa ni mpini juu ya mpini.
Pamoja na nipe dili pia kuna nyimbo nyingine kama Singida Dodoma,Mida Mibovu na nyingine kibao zinazopatikana katika album yake mpya ya "Nge 2800".
Pia ameeleza kua tayari ameshafanya video ya Nipeni dili kupitia kampuni ya Visual Lab na muda wowote kuanzia sasa itakua hewani.

No comments: