Wednesday, November 19, 2008

"Pro Jay Kwenda Nigeria Leo".


MWANAMUZIKI maarufu wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘ Profesa Jay’, anaondoka nchini leo kwenda Abuja, Nigeria kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards with Zain (MAMA).
Watakaochuana kuwania tuzo na Profesa Jay katika kundi la Hip Hop ni pamoja na TheGame na Lil Wayne kutoka Marekani, pamoja na HHP kutoka Afrika Kusini na 9Icekutoka nchini Nigeria.
Tuzo za Muziki za Afrika MTV/Zain (MTV Africa Music Awards with Zain) (MAMA) ni shoo mpya ya tuzo ambayo imeandaliwa na MTV kuenzi na kusherehekea muziki na utamaduni wa Afrika.
Tuzo za MTV Africa Music Awards with Zain zinaonyesha aina ya muziki unaopendwa na vijana, watazamaji wa MTV, kituo kinachotazamwa na zaidi wa watazamaji milioni 50 katika Afrika.
Tuzo hizi zimeadaliwa kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya musiki wa wasanii Waafrika ndani na nje ya Afrika na ni fursa ya aina yake ya kuwaonyesha washabiki wa muziki wasanii wa Afrika na Kimataifa wanaotingisha dunia.
Washiriki wengine wa tuzo hizo ni pamoja na wasanii pacha wa Nigeria wa R&B ,P-Square.
Tuzo hizo ni pamoja na Kundi Bora, Video Bora, Msanii Bora wa Jukwaani, Mkali wa R&B, Msanii wa Mwaka

No comments: