
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Sir Juma Nature hivi karibuni amekwisha ikamilisha albamu yake ya tano itakayoitwa Tugawane Umasikini itakayokuwa na jumla ya nyimbo 12.
Juma Nature amezitaja nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo ambayo amekiri wazi itakuwa ni ya kuotea mbali, kuwa ni Ofisa salama,Nimeshakwama,kukakaa maskani,siku za wiki,Burudika,nitakuwa mgeni wa nani na wimbo wa kilichokusibu.
Juma Nature mpaka sasa amekwishatoa albamu nne ambazo ni Nini Chanzo,Ugali, Ubinadamu kazi pamoja na albamu ya Historia.
No comments:
Post a Comment