
Mastaa kadhaa wa muziki kutoka Marekani wanatarajia kudondoka Bongo Dec 3 kwa ajili ya show ya kufa mtu kwenye tamasha linalofanyika kila mwaka lijulikanalo kama likizo Tyme.
Mastaa hao hatari, Joe Thomas, kundi maarufu la muziki wa R&B la Boyz II Men, wakali wa muziki wa ragga, Devonte na Tanto Mentro,mwanadada Tanya Stephan, watakamua kwenye tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Leaders' Club Dec 5.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Entertainment Masters Limited, Hellen Sweya, akiongea na Itajulikana lengo la kuwaleta wasani hao nyota ni kutoa fursa kwa Watanzania wa rika zote kupata burudani safi ya hadhi ya kimataifa. “Tunaahidi tamasha hilo litakuwa tofauti na matamasha yaliyopita ya Likizo Tyme kutokana na maboresho makubwa kuanzia waandaaji na onyesho lenyewe kuwa na jukwaa la hadhi ya kimataifa,” alisema Hellen.